Monday, January 17, 2011

Kengele

Nina sikia kengele ina pigwa kengele
Wakati ume fika kupiga kengele , kengele
Nasi tupige hatua wakati unasikia kengele
Kengele, kengle usibaki wapopiga kengele


Kengele umepigwa basi sisi tusongembele
Mistari yamechorawa tuyavuke twende mbele
Hii vibe ya kurudishwa nyuma hatutaki
Kama hamna maendeleo bora basi hatutaki
Tumefahamika na kuelimika na hatutaki mabaki
Wakati hii situ kupinduliwa calenda bali ni a hatua
Mabadiliko maishani yana anzaa hatua kwa hatua
Bidii tumetia na hamna mafanikio
Nikama watu wamelalia masikio
Huku kufanaya kazi bila mafanikio
Kengele imepigwa, shida lazima iwe ime kamilika
Sibaki nyuma mpaka hii struggle ime kamiliaka
Juliani alitueleza tuwache usingizi yani Rauka
Mimi nina waahidii sisi sote tuwe tume rauka
Nimetazama shida yametukumba bila aibu
Tusipigane juu ya watu wasiofaa nit tu aibu

Nina sikia kengele ina pigwa kengele
Wakati ume fika kupiga kengele , kengele
Nasi tupige hatua wakati unasikia kengele
Kengele, kengle usibaki wapopiga kengele


Tuwachane na mapenzi ya godoro
Tuwe macho tutatuwe hii migogoro
Macho ya funguke tuone ukweli hatuoni
Wale waliochaguliwa wame tuziba hatuoni
Wasiweze kunichukia haya tu ni maoni
Sina hela ya kujikinga na wanao Linda mwili
Tukumbuke kila tutendayo ina athari kwa mwili
Kengele, kengele , kengele imesikika
Kote inchini kwenye milima na mabonde imesikika
Usingizi lazima ikamilike, hatua ichukuliwe
Inchi ni yetu na tunafaa kulinda isichukuliwe
Na wale walio namali, walio panga kuchukua
Kengele kengele, kengele, hatua tuna chukua
Hatuwachi inchi iharibike na kukosa mwelekeo
Kama sauti moja tungane natuweze kupeana mwelekeo
Tusipote na tu itike wito wa kengele.

Nina sikia kengele ina pigwa kengele
Wakati ume fika kupiga kengele , kengele
Nasi tupige hatua wakati unasikia kengele
Kengele, kengle usibaki wapopiga kengele