Wednesday, April 2, 2008

Swahili

Moyo umekua mwepesi, sabau ya vitu vingi tumevitupilia mbali. Wakati wowote ule unapohitaji vitu fulani, bidii ni kitu cha lazima. Kenya ni inchi ya watu wengi wenye kabila mbali mbali. Na wenye mali na hali mbali mbali. Mimi hoja kuu nikukua mkali mithili ya pili pili. Ukipita mahala flani unawawacha watu waki lia nikama wakati vitungu vinatayarishwa. Sitaki kuonekana nikama nimepoteza wanaosoma mawazo haya lakini kuaelimisha kwa kiwango flani. Ndiyo badaye nisikiye flani wa flani alibarikiwa kwa kusoma yale maandishi niliyoandika. Lugha ni mgumu mno lakini ni bora kushida kutosoma am kuandika mawazo niliyonayo. Nataka niwemarufu kwenye msafara, jina liweze kungara msafada, litambulike kati ya majina marufu duniani. Wakati Professor Jay, Juma Nature na Solo Thang wanapoitwa, jina langu liweze kutajwa wakati huo. Mimi si mwana bongo lakini ni kujaribu tu kutunza tamaduni hilo njema. Kusema ninaweza kusema mpaka keshona hayo yote yawe yenye vina na maana lakini lile nililopenda haliwezi kwenda. Walinena kuwa siwezi andika swahili lakini nipo na hata sijashtuka akamwe. Nitalichambua lugha ubaki umeshangaa. Ah! Umezubaa, nabado niko nimchanganyiko ya vitu vingi duniani. Mtu wa kabila langu haweze kuandika lugha jinsi hii, hapana. Ni mapendeleo niliyonayo moyoni. Hebu tazama jamani, fani blia mimi itakua nikama utani, basi hamna mahali niendapo, niko mahala humu, ndani ya fani yani nimedunga hema, nime tia nanga na niko tayari na njora kujilinda, kujikinga kwa wale wanaofikiri mimi ni wa makamo na sifai mahali humu. Watu wa makao wafanya fani yangara, na Professor Jay aliwasimulia. Jamani kuweni makini ni bora kusikia kushinda kutosikia na kupotea, hamja sikia elimu ni nguvu basi tia fora, tia manani kwa kila utendacho, kwa vile maisha tunayoishi si yetu sisi bali ni kwa wakati huo huo kisha itatoweka. Mahala upo na ulifikia mshukuru Mola. Jamani nie andika…..

Emigee's ish

No comments: