Wednesday, November 26, 2008

B.U.G (Bado Tuko Gizani)

siku ya leo, nikama yale mengine/
hamna tofauti yeyote kama yale mengine/
kama ni jua, imewaka nikama kawaida/
shida ndiyo hayo yametukumba moja baada ya nyingine/
sijui niuzike kichwa kwenye mchaga/
ama ni weze kupata kujificha kwa kanga/
uzito huu umenilemea mimi mno/
fitina umeenea kote kote, nikama maji ya mafuriko/
tarajiyo nikuliona siku mpya, siku njema/
siku bila magereza, kwa vile hakuna uhalifu/
siku bila askari, na bila polisi haramia/
siku bila daktari, kwavile hamna wagonjwa/
siku bila dini tofauti. kwavile dini iliopo ni kupendana/
ninafahamu vyema siku kama hii ni ndoto/
shida ni kuwa sisi hatupati wakati wakulala/
ndiyo tuweze kupata ndoto ya kunene/
Rais Obama na wana-amerika wamepata ukombozi/
juu ya ndoto walioota wao/
mbona tusiweze tu kupendana? kuonyeshana upendo?
tuweze kuishi kwa amani? tuwache fitina ya makabila?
kwa hakika tuke mbali sana kupata uhuru wa hakika/
uhuru tulionalo ni ya bendera tu kupepea angani/
bado tuko jangwani, na hatuwezi ota mimea ya mafanikio/
kwa wakati mwingine mimi hujihisi nikama najihurumia kuwa Mkenya/
kwa vile hii maisha bila uvumilivu hakwepo/
bado tuko gizani. B.U.G hata kwenye mwangaza bado tuko gizani...

No comments: